Viazi mviringo ni zao linalotokana na zaomzizi wa kiazi. Zao hili kwa kitaalam huitwa solanum tuberosum.
Asili yake ni Peru na Bolivia
Kwa Tanzania, zao hili hulimwa Moro, mbeya, iringa, Kilimanjaro, tanga njombe, songwe na arusha.
MAHITAJI MUHIMU YA ZAO HILI
¤joto kati ya nyuzi 25-30.
¤mvua kiasi cha mm 450 kwa kipindi chote cha ukuaji.
¤udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji.
AINA ZA VIAZI MVIRINGO.
¤Dutch robijn. Kutoka Holland.. Huvumilia uginjwa was ukungu,, hushambuliwa sana na mnyauko bakteria, hipendwa na walaji wengi
¤roslin. Kutoka Scotland. Ngozi yake ni nyeupe,, ndani ni nyeupe, huvumilia ugonjwa was ukungu.
¤Kerr's .. Ngozi yake ni nyekundu,, ndani ni nyeupe,, hushambuliwa sana na mnyauko bakteria.
¤uyole. Kutoka kituo cha utafiti cha KILIMO Uyole. Kuna aina zake kama baraka,, sasamua, tana na bulongwa.
UANDAAJI WA MBEGU.
Tumia mbegu zenye umbile dogo kama yai, hifadhi kiasi cha robo tani,, hifadhi eneo lenye mwanga hafifu. Hakikisha zimechipua vizuri na hazina magonjwa wala wadudu.
UANDAAJI WA SHAMBA NA UPANDAJI MBEGU.
¤lima na kusawazisha kuondoa magugu na mabaki ya majani.
¤weka mbolea na changanya vizuri.
¤andaa matuta umbali wa sm 75 kutoka tuta hadi tuta.
Panda mbegu kipindi ambacho mvia huanza kunyesha. Umbali wa miche ni sm 30 ma mistari ni sm 75. Fukia kina cha sm 10.
¤tumia mbolea ya kupandia CAN /DAP gram 5 kwa kila shina.
PALIZI NA MATUMIZI YA MBOLEA.
¤palilia kila magugu yanapojitokeza. Hakikisha unajaza udongo kwenye mashina ya viazi.
Weka mbolea ya kukuzia aina ya NPK (yaramila winner) kwa kipimo sawa na cha kupandia.
¤mwagilia kwa wiki Mara mbili kwa kipindi ambacho hakina mvua.
MAGONJWA NA WADUDU.
¤mbawakavu. Tumia dawa aina ya Malathion au thiodan.
¤ukungu. Tumia dawa aina ya radomil au karate.
MAVUNO.
¤uvunaji hufanyika miezi 3-5 baada ya viazi kupandwa.
¤hakikisha baada ya mavuno viazi havihifadhiwi kwa muda mrefu ili kuzuia visiote.
¤hekari moja hutoa tani 6-8 za viazi.
Comments
Post a Comment