KILIMO BORA CHA MUHOGO.

Muhogo ni miongoni mwa mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula hasa maeneo yenye mvua kidogo na sehemu zenye ukame. Muhogo hutumika kama zao la kinga ya njaa ambapo mizizi yake hutumika kama chakula na majani yake kama mboga. Zao hili hulimwa sana mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Mara na Mwanza. Muhogo ni moja kati ya mazao yanayohimili ukame wa muda marefu na hivyo kusisitizwa na
wataalam wa kilimo kuwa kama kinga ya njaa.
MAHITAJI MUHIMU YA ZAO LA MUHOGO.
✍Zao la muhogo linahitaji joto la wastani kama joto la ukanda wa Pwani.
✍Zao pia linahitaji rutuba ya wastani, udongo tifutifu au kichanga na mvua ya wastani.
✍Unyevunyevu ukizidi na mbolea kuwa nyingi husababisha mihogo kuku asana sehemu ya juu na kutoa majani mengi.
✍Udongo ukiwa mzito sana na wenye kutuamisha maji, mihogo itashindwa kutengeneza kiazi (tuber) itakiwavyo.
✍Sehemu zenye mawe pia huzuia mizizi kukua na kuvimba vizuri.
✍Ardhi ya chumvichumvi hufanya mihogo mitamu kuwa michungu.
AINA ZA MIHOGO.
Kuna aina mbalimbali za mihogo. Baadhi ya sifa zinazoangaliwa wakati wa kutayarisha mbegu za mihogo ni;
✍Muda wa kukomaa.
✍Muhogo mtamu au mchungu.
✍Wingi wa mavuno.
AINA ZA MIHOGO MITAMU.
✍Kibaha.
✍Aipin.
✍Kigoma.
✍Kigoma red.
✍Msitu Zanzibar.
✍Kiroba.
✍Binti Athumani.
✍Mzungu.
MIHOGO MICHUNGU.
✍Liongo.
✍Ali mtumba.
✍Mapangano.
✍Luanda.
✍Mzimbatala.
✍Lumbago.
KUANDAA SHAMBA NA KUPANDA MBEGU.
✍Lima na kusawazisha vizuri shamba ili kuondoa magugu na majani yote.
✍Kama eneo lina maji mengi, tengeneza matuta yenye upana wa sm60.
✍Chagua mbegu bora zisizokuwa na magonjwa na zikate katika pingili zenye urefu was m 25 – 30.
✍Mbegu ziwe na wastani wa macho matano na unene was m 3. Mara nyingi sehemu ya shina ndiyo inayofaa kukata mbegu.
✍Panda kwa umbali wa mita 1 kwa mita 1 katika kilimo cha sesa na mita 1 kwa sm 75 katika kilimo cha matuta.
✍Epuka kupanda pingili change na zilizozeeka.
✍Hakikisha macho mawili yako ndani ya ardhi ili kutoa mizizi.
✍Panda pingili kwa kulaza kidogo (nyuzi 45) na macho yatakayotoa majani yaelekee juu.
✍Gandamiza kidogo udongo ili pingili ishike vizuri.
✍Palilia mapema. Mihogo inapokuwa hufunika ardhi hivyo kuzuia majani kuota na kukua vizuri.
✍Matumizi ya mbolea hayashauriwi kwani mihogo hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya wastani.
MAGONJWA NA WADUDU.
✍Batobato (cassava mosaic).
✔Husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe.
✔Majani ya mmea ulioshambuliwa huwa na rangi ya njano na kukosa umbo maalumu.
   ☑Kuzuia.✔
✍Panda vipandikizi ambavyo havijatoka katika mmea ulioathirika na ugonjwa huu.
✍Chovya mbegu ulizokata kwenye maji ya moto kwa muda mfupi na taadhari kubwa.
✍Tumia dawa aina ya KARATE  kuua nzi weupe.
✍Buibui wa mihogo (cassava  green mite) na vidung’ata (cassava mealy bugs).
✔Majani ya mihogo hunyauka na kudumaa kwa mmea.
✔Shina la mmea huonekana limezungukwa na utando mweupe (white mealy wax).
✔Shina la mmea huonekana limepinda.
✔Majani ya mmea hupukutika.
✔Mmea unaweza kufa kama tiba isipopatikana kwa haraka.
        ☑Kuzuia.✔
✍Tuma dawa aina ya DIMETHOATE.
✍Panda mbegu ambazo bado hazijashambuliwa na wadudu hawa.
UVUNAJI.
✍Mihogo hukomaa kuanzia miezi sita hadi tisa na kuendelea kulingana na aina ya mohogo.
✍Ikiwa mihogo yako imekomaa, ing’oe yote.
✍Epuka kuweka kidonda katika muhogo unaovuna ili kuepusha kuoza haraka.

Comments