Nyanya ni zao la biashara na chakula. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote yaani masika na kiangazi.
Nchini Tanzania, zao hili hilimwa kwa wingi mikoa ya mwanza, iringa, morogoro, mbeya, tanga na pwani..
MBEGU BORA ZA NYANYA..
◇tengeru'97. Huvumilia baadh ya magonjwa,, ina ganda gumu hivyo haiharibiki kirahisi. Huzaa sana.
◇tanya. Hazaa sana lakini siyo kama tengeru. Haina matunda makubwa sana. Ladha yake nzuri na hupendwa na watu wengi.
◇assila F1. Huzaa sana. Huvumilia magonjwa na hali ya hewa. Ina ganda ladha nzuri.
MAHITAJI YA NYANYA..
◇joto kati ya nyuzi 24-30.
◇mvua za wastani.
◇udongo usiotuamisha maji na wenye rutuba ya kutosha.
UANDAAJI WA SHAMBA NA UPANDAJI MBEGU.
◇andaa shamba mwezi mmoja au miwili kabla ya kupanda.
◇baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo na ondoa magugu yote shambani.
◇andaa mashimo kutegemeana na miche iliyopo.
◇mwagilia shamba siku moja au mbili kabla ya kupanda miche..
◇hamisha niche kutoka kitaluni baada ya kufikia urefu wa sm 15.
◇panda kwa nafasi ya sm 60 kati ya mche na mche na sm 70 kati ya mistari.
◇baada ya hapo mwagilia maji kidogo ili kufanya miche isimame imara shambani.
Note:
◇nyanya huitaji maji mengi ili kuzaa matunda mengi na yenye afya. Mwagilia NYANYA mara mbili au tatu kwa wiki kutegemeana na aina ya udongo.
◇usituamishe maji shambani.
PALIZI NA MATUMIZI YA MBOLEA.
◇palilia wiki ya pili baada ya kupanda. Endelea kupalilia Mara kwa Mara kuweka shamba katika hali ya usafi.
◇weka mbolea ya kukuzia ya NPK baada ya kupalilia. Endelea kuweka mbolea hii katika kipindi cha mavuno ili kurefusha kipondi cha mavuno.
MAGONJWA NA WADUDU.
◇bakajani. Majani hiwa na ukungu was kijani au mweupe na kisha hukauka. Tumia RIDOMIL, BRAVO FUNGARAN, MILRAZ,..
◇rasta (yellow leaf curl). Nyanya hupasuka, mimea hudumaa na majani hushambuliw na kuwa na rangi ya njano au zambarau. Tumia SELECROM, DURSBURN, ACTELIC..
MAVUNO.
◇vuna wakati nyanya zimekomaa kabisa lakini bado zina rangi ya kijani,
◇tenganisha tunda na kikonyo na sio kikonyo na shina,
◇vuna wakati wa asubuhi na jioni.
◇baada ya kuvuna weka nyanya kwenye vyombo vilivyo wazi kama matenga na weka kivulini.
◇uza nyanya zako.
◇hekari hutoa tani 7-9.
Assila f1 tan 25 kwa eka
ReplyDelete