KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI

Vitunguu maji ni zao la mbogamboga ambalo hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Hulimwa zaidi nyanda za baridi na joto kiasi. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa sana Singida, Morogoro, Arusha na Iringa. Joto kiasi linatakiwa kwa ajili ya ukuaji wa balbu zake.. Joto likizidi, vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaotakiwa.

UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI..

udongo wowote wenye rutuba na usiotuamisha maji.
hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo.
kwenye udongo wa mchanga mwingi, umwagiliaji wa Mara kwa Mara ni lazima.
maji mengi yanahitajika wakati wa vitunguu kutengeneza balbu.
unyevu ukizidi ardhini, balbu huweza kuoza.

UZALISHAJI NA UPANDAJI.

Lima na kutifua vizuri ili kuondoa mabaki ya mimea na vipande vikubwa vya udongo.
tengeneza matuta yenye upana wa mita moja.
panda vitunguu moja kwa moja shambani au kutoka kitaluni. Umbali wa mmea na mmea no sm 10 na mstari hadi mstari ni sm 15.
kama ukiamua kutengeneza kitalu, hakikisha miche inakaa kwa wiki 6 ndipo ihamishiwe shambani,. Kwa muda wote huo, angalia kitalu kwa ukaribu sana.

AINA YA VITUNGUU.

red creole.
Bombay red.
hybrid F1.

Note:
palilia kwa mkono na Mara kwa Mara.
kumbuka kuweka matandazo baada ya kupalilia.
vitunguu hufanya vizuri kama shamba likiwekewa samadi au mboji iliyoiva vizuri.

UVUNAJI.

uvunaji ufanyike kuanzia siku 90-120.
vuna kwa mkono (kung'oa kwa mkono). Dalili za kukomaa ni majani kuanguka.
hekari moja hutoa kati ya tani 7-9.
tunza kwenye joto  la kati ya nyuzi 4-10. Vitunguu vikitunzwa vizuri hukaa hadi miezi tisa bila kuharibika.
uza vitunguu vyako baada ya bei kuwa nzuri.

Comments